Kocha Mkuu wa Chelsea, Mauricio Pochettino, amesema watu wasiwe na wasiwasi juu ya kiwango cha timu yake kwani bado anaitengeneza kuja kuwa bora zaidi.
Chelsea ambayo kwa sasa ipo nafasi ya 14 kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England, imekuwa haina matokeo mazuri msimu huu ikishinda mechi moja pekee kati ya sita.
“Ni vigumu kuliko nilipokuwa Southampton na Tottenham, niamini,” alisema kocha huyo ambaye aliwahi kuzinoa timu hizo.
Tunafanya vizuri zaidi hapa, lakini tunakosa jambo muhimu zaidi katika soka, nalo ni kufunga.”
Kuhusu kwa nini ilikuwa ngumu zaidi kwa Spurs, Pochettino alisema: “Tulikuwa tukifanya kazi kubadili na kubuni mkakati. Hapa, mpango ulikuwa tayari umefanywa.
“Naamini tutakaa sawa, tuwe na subira na kuangalia namna wachezaji wote ambao ni majeruhi wapone.
“Kila mtu anaweza kusema kwamba mpango huo si sahihi, lakini ninaamini sana katika mradi huu. Tunahitaji muda tu kubadili mtazamo huo kwa sababu siku si nyingi tutaenda kubadili mtazamo wao.
Pochettino anajaribu kujenga hali ya kujiamini kwa wachezaji wake, ambao wengi wameonekana kutojiamini akiwemo Mykhailo Mudryk.