Kocha Mkuu wa Coastal Union Mkenya, David Ouma amesema mwanzo mzuri ndani ya kikosi hicho ni kutokana na ushirikiano mkubwa anaoupata kutoka kwa viongozi huku akiwamwagia sifa wachezaji kwa kuyafuata maelekezo yake vizuri uwanjani.

Ouma aliyeteuliwa Novemba 9, mwaka huu kukiongoza kikosi hicho akichukua nafasi ya Mwinyi Zahera aliyepelekwa kuwa Mkurugenzi wa Programu za vijana ameingoza timu hiyo katika michezo mitatu ambapo kati yake ameshinda miwili na kupoteza mmoja tu.

“Tuko kwenye wakati mzuri kwa sababu kupata pointi sita kati ya tisa sio jambo dogo, bado tuna nafasi ya kufanya vizuri zaidi ya hapa kwani wachezaji wanaonyesha uwanjani kwa vitendo, naamini tukiendelea hivi tutafikia malengo,” amesema.

Tuna washambuliaji ambao wanaweza kufunga mabao mengi hivyo nitaendelea kukaa nao na kuwajenga zaidi kwa sababu hata ukiangalia mchezo wetu na Singida Big Stars tuliopoteza mabao 2-1, ni utulivu tu ulikosekana eneo la mwisho,” amesema.

Baada ya ushindi wa mabao 3-1, ilioupata dhidi ya Geita Gold, kikosi hicho kinajiandaa kuwavaa Kagera Sugar, Jumamosi (Desemba 09), katika Uwanja wa CCM Mkwakwani jijini Tanga.

Dkt. Tulia awajulia hali majeruhi wa maafa Hanang'
Arteta aweka ngumu usajili wa Ramsdale