Carlos Alos Ferrer kwa muda mrefu amekuwa katika presha kubwa tangu timu ya taifa ya Rwanda ‘Amavubi’ iondolewe kutoka katika mbio za kufuzu za Mashindano ya Mataifa ya Afrika (Afcon 2023) baada ya kuchapwa mabao 2-0 na Msumbiji katika mchezo wa Kundi L.

Lakini kocha alitangaza uamuzi wake wa kujiuzulu kupitia katika ukurasa wa Instagram baada ya kushindwa kuiongoza timu hiyo kufuzu kwa Fainali za AFCON 2023.

Mambo yaliharibika zaidi kwa kocha huyo wakati kiongozi wa zamani wa Chama cha Soka cha Rwanda, Olivier Nizeyimana alipojiuzulu Aprili 2023, akidai kuwa amezidiwa na majukumu binafsi.

Lakini inaaminika kuwa Nizeyimana alilazimisha kuondoka baada ya Rwanda kupoteza pointi kijinga walipocheza dhidi ya Benin jijini hapa kwa kumchezesha mchezaji asiyehalali Kevin Muhire.

Matokeo hayo yalimuacha kocha Ferrer akiwa na kibarua kizito cha kuifunga Msumbiji na Senegal.

Tumekuja kushindana katika mechi za kufuzu kwa AFCON 2023, na sasa ndio muda wa kuanza mipango mipya kwa wanachama wapya wa shirikisho, na hata kwangu, ni wakati wa kuanza miradi mipya,” ameandika Ferrer.

Bilioni 10.99 zatumika kuboresha miundombinu ya Elimu
KMKM, JKU kuhamia Dar es salaam