Kocha Mkuu wa Young Africans, Miguel Gamondi, ameuomba uongozi wa klabu hiyo kumtafutia mechi ya kirafiki ili kukipima kikosi chake kabla hakijavaana na CR Belouizdad ya Algeria.

Timu hiyo itavaana na CR Belouizdad ljumaa ya wiki ijayo katika mchezo wa kwanza wa kundi D wa Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL, utakaopigwa Katika Uwanja wa 5 July 1962, Algeria.

Katika Kundi hilo, Young Africans imepangwa na CR Belouizdad, Medeama ya Ghana na Al Ahly kutoka Misri.

Akizungumzia maandalizi ya kikosi chake Kocha Gamondi amesema anahitaji mchezo wa kirafiki kabla ya kuvaana na Belouizdad ili kukiweka sawa kikosi chake.

Tumepata mapumziko kutokana na ligi kusimama kwa mechi za timu za taifa, tunafanya sana mazoezi kuhakikisha tunakuwa bora katika mchezo ujao, tunahitaji mchezo wa kujipima nguvu.

“Nimezungumza na viongozi watafute timu ambayo itatupa ushindani tucheze nao Jumamosi, baada ya mchezo huo ndiyo tutafanya mazoezi ya mwisho kuelekea mchezo huo mkubwa,” amesema.

Kocha huyo kutoka Argentina amesema tayari ameanza kuifuatilia CR Belouizdad na kubaini ubora na udhaifu wao.

Mnagombana kila siku, haina faida - Waziri Mkuu
Mlinda Lango Chelsea matumaini kibao 2023/24