Kocha Mkuu wa Geita Gold FC, Fred Felix Minziro amesema wapo tayari kwa mchezo wa Robo Fainali Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’ dhidi ya Mabingwa watetezi Young Africans.

Geita Gold FC ambayo iliwasili jijini Dar es salaam katikati ya juma hili, imekuwa katika mkakati mzito wa kutaka kuizima Young Africans katika mchezo huo na kufuta uteja dhidi ya miamba hiyo ya Jangwani.

Kocha Minziro amesema tayari ameshawapa mbinu zote wachezjai wake, kwani anajua wanakutana na vigogo, lakini wamejipanga kupambana kiume ili kupata ushindi kwa mara ya kwanza mbele ya Young Africans, aliyokiri ina kikosi imara.

“Huwa nawaambia wachezaji kutorudia makosa ambayo wameyafanya katika michezo iliyopita hii ndio njia pekee wanaweza kushinda kama watarekebisha makosa, matumaini yetu ni kufanya vizuri kwani hatuishi na matokeo ya yaliyopita kwani mchezo huu kwao ni mpya kabisa,” alisema kocha aliyewahi kuwa nyota na kocha wa Young Africans sambamba na kuzinoa timu nyingine kadhaa nchini.”

Kwa upande wa beki Geita Gold FC, George Wawa amesema; “Kambini tukikaa tunapeana mikakati ya kupambana kwa nguvu na kuhakikisha tunapata matokeo mazuri. Huu sio mchezo rahisi ukizingatia walitufunga mara ya mwisho tulivyokutana nao.”

Young Africans itakuwe mwenyeji wa mchezo huo utakaopigwa Uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es salaam kesho Jumamosi (April 08), huku ikikumbukia namna ilivyowaadhibu wababe hao wa mkoani Geita kwa mabao 3-1 kwenye mchezo wa Ligi Kuu mwezi uliopita uwanjani hapo.

Kashfa ya mabati: Waziri, kaka yake kula Pasaka Jela
Wakulima, Wavuvi wapatiwa mkopo wa Bilioni 78.54