Kocha Mkuu mpya wa Geita Gold FC, Hemed Suleiman ‘Morocco’ amesema lengo lake namba moja msimu ujao wa ligi kuu Tanzania bara ni kuhakikisha timu hiyo inamaliza katika nafasi nne za juu (Top Four).

Akizungumza kutoka Morogoro ambapo timu hiyo imeweka kambi kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao, kocha huyo aliyechukua nafasi ya Fred Felix Minziro aliyetimkia Prisons, amesema kwa usajili walioufanya na mazoezi ambayo amekuwa akiwapa wachezaji wake, ana imani kubwa ya kufikia lengo hilo.

“Nimeanza vizuri, wanajaribu ambacho ninawafundisha, nawashukuru wao na viongozi wa klabu hii pia, malengo yetu ni kuona msimu ujao tunafanya vizuri zaidi kuliko wachezaji kuzoea kile msimu uliopita, naamini kwa jinsi tulivyofanya usajili na wachezaji waliopo hapa kitu hicho kinawezekana kabisa,” amesema Morocco.

Kikosi hicho kimepiga kambi Morogoro tangu Julai 19 kujiandaa na msimu mpya na inatarajia kumaliza Agosti mbili na kurejea mkoani Geita kwa maandalizi ya mwisho kabla ya kuanza kwa ligi kuu Tanzania Bara msimu wa 2023/24 Agosti 15.

Msimu uliomalizika Geita Gold ilimaliza ligi ikiwa nafasi ya saba ikivuna 37 na hivyo kushindwa kupata nafasi ya kushiriki michuano ya kimataiafa kama ilivyokuwa msimu wa 2021/22.

Msimu wa 2021/22, Geita Gold ilimaliza nafasi ya nne ikiwa na pointi 46 na kukata tiketi ya kucheza michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika ambapo ilitolewa na Hilal Al Sahil ya Sudan katika hatua za mwanzoni.

Kai Havertz: Sina uhakika wa kucheza Arsenal
Messi amshangaza Rais FC Barcelona