Kocha Mkuu wa Geita Gold, Felix Minziro ametangaza hali ya hatari kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kusema kuwa kwenye michezo ambayo imebaki watafanya kweli kupata matokeo.
Minziro alisema kuwa wanatambua wana kazi kubwa kwenye michezo iliyosalia , lakini ameahidi kuhakikisha wachezaji wake wanapambana na kufanikiwa kupata alama tatu muhimu.
“Kuna michezo ambayop imesalia kwa ajili ya kukamilisha mzunguko wa pili, hii michezo huwa inakuwa migumu kutokana na timu zote kucheza kwa juhudi kutafuta matokeo.”
“Kutokana na maandalizi ambayo tunafanya tunaamini matokeo tutapata kwani
mchezo wetu uliopita tulipoteza dhidi ya Tanzania Prisons hapo tunafanyia kazi makosa ili kushinda,” amesema Minziro.
Geita Gold imebakiwa na michezo mitatu ambapo mchezo wao ujao unatarajiwa kuwa dhidi ya Mbeya City.
Hadi sasa timu hiyo yenye maskani yake mkoani Geita imefikisha alama 37 ikiwa nafasi ya tano, huku ikicheza Michezo 27 kwenye ligi.