Kocha Mkuu wa Singida Big Stars Hans Van Der Pluijm amesema yupo tayari kupambana na Young Africans katika mchezo wa mwisho wa Kundi B, katika Michuano ya Kombe a Mapinduzi inayoendelea Kisiwani Unguja ‘Zanzibar’.

Young Africans jana Jumatano (Januari 04) iliibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya KMKM, huku Singida Big Stars ikitangulia kuifunga 2-0 KMKM Jumatatu (Januari 02), hivyo kulifanya Kundi B kuwa na changamoto ya kumpata mshindi atakayetinga Hatua ya Nusu Fainali.

Kocha Hans ambaye alikua akiifuatilia Young Africans Uwanja wa Aman amesema amewaona wapinznai wake na ameshajua mapungufu yao, ambayo atayatumia kushinda mchezo wa kesho Ijumaa (Januari 06).

“Kupangwa kundi moja na Young Africans ni furaha kwangu napenda kucheza na timu kubwa kwa sababu zinatoa ushindani wa kweli na mimi nimekiandaa kikosi kushindana mchezo wetu na wao natarajia ushindani,”

“Nimewafuatilia mwanzo mwisho, nimewaona wana timu nzuri waliokuja nayo hapa Zanzibar, nimeona madhaifu yao na mazuri yao pia, nitakiandaa vizuri kikosi chake katika maozezi ya mwisho ili kupambana nao na kupata ushindi.”

“Makosa tuliyoyafanya kwenye Mchezo wa Ligi Kuu Bara kwa kukubali kipigo cha mabao mengi hatutarajii kuyarudia huku kwa sababu tunacheza michezo ya mtoano na lengo letu ni kufika mbali, tunataka alama katika michezo yote.” amesema Kocha huyo kutoka Uholanzi

Singida Big Stars inaongoza Msimamo wa Kundi B, kwa tofauti ya mabao ya kufunga, huku Young Africans ikishika nafasi ya pili kwa kuwa na alama tatu na bao moja la kufunga, huku wenyeji KMKM wanaburuza mkia kwa kupoteza michezo yote miwili.

Watano wang'olewa Ihefu FC
Ally Kamwe: Nilishangaa alichoniambia baba