Kocha Mkuu wa Ihefu FC John Simkoko amesema suala la kuhamishwa kwa mchezo wa Robo Fainali Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ dhidi ya Simba SC, halitomzuia kufanya alichokidhamiria na kutinga Nusu Fainali ya Michuano hiyo.

Ihefu FC italitarajia kukutana na Simba SC Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam kesho Ijumaa (April 07) lakini italazimika kwenda Azam Complex, Chamazi baada ya Shirikisho la Soka ‘TFF’ kufanya mabadiliko hayo.

Kocha Simkoko amesema kubadilishwa kwa uwanja hakuwezi kuathiri kikosi chake kutokana na maandalizi mazuri waliyoyafanya kwa sababu hata kabla ya hapo isingekuwa mchezo mwepesi.

Amesema wamejiandaa kupambana na kushinda na kikubwa mazingira watakayochezea ni jijini Dar es salaam, hivyo haijalishi Uwanja gani ambao utashuhudia wakipambana na miamba hiyo kutoka Mtaa wa Msimbazi jijini humo.

“Dhamira yetu ni kupambana katika Uwanja wenye vigezo vya kupambana, kuhamishwa kwa uwanja hakujabadilisha chochote, sisi tumejiandaa kukakabili Simba SC na kupata ushindi.”

“Tangu mwanzo tulifahamu mchezo huu utachezwa Dar es salaam, kwa hiyo hata huko Chamazi bado ni Dar es salaam, kwa hiyo niwatowe hofu mashabiki wa Ihefu FC kuhusu mabadiliko hayo.” Amesema Kocha Simkoko

Uwanja wa Uhuru kesho Ijumaa (April 07) utakuwa na matumizi mengine na kulazimisha waandaaji wa michuano ya ASFC, Shirikisho la Soka ‘TFF kufanya mabadiliko ya Uwanja.

Sababu kubwa za mabadiliko hayo ni kutokana na Uwanja wa Uhuru uliopangiwa kutumika kwa shughuli za mashindano makubwa ya usomaji wa Quran tukufu, ambapo kesho utakuwa ukiandaliwa kwa ajili ya Mashindano hayo yatakayofanyika Jumapili (April 09).

Kocha Stars amrudisha Fei Toto Young Africans
Simba SC yakubali kupelekwa Chamazi