Kocha Mkuu wa JKT Tanzania, Malale Hamsini amesema dakika 90 za mchezo wa Ligi Kuu unaopigwa kesho Jumanne (Agosti 29) dhidi ya mabingwa watetezi Young Africans, ndio zitaamua matokeo kwani wamejiandaa kushindana na wala hawatishwi na matokeo wanayopata wapinzani wao hao ambao wamefunga mabao 10 katika mechi zao mbili zilizopita za michuano yote.

JKT Tanzania itakuwa mgeni wa Young Africans kwenye Uwanja wa Azam Complex mechi itakayopigwa kuanzia saa l:00 usiku, ikiwa imetoka kushinda mchezo wa kwanza dhidi ya Namungo FC.

Kocha Malale amesema wamekuja Dar ili kuendeleza pale walipoishia lengo likiwa ni kukusanya alama tatu muhimu.

Amesema wanatambua wanaenda kukutana na timu inayotetea taji la Ligi na iko katika bora, lakini na wao ni bora pia.

“Kila timu ina wachezaji 22, tunajuana huko huko kwani hata sisi ni bora na dakika 90 zitaamua na aliyejiandaa vyema ndiye ataibuka na ushindi,” amesema.

Young Africans katika mechi zake mbili zilizopita Young Africans imefunga jumla ya mabao 10-1, wakiifunga KMC 5-0 kwenye Ligi Kuu Bara na kisha kuifunga 5-1 Asas ya Djibouti katika mechi ya hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika juzi Jumamosi (Agosti 26).

Walimu wathaminiwe: DC Hamid Seif
Azam FC kujiuliza tena leo