Kocha Mkuu wa Kagera Sugar Mecky Maxime, amesema amejipanga kufanya vizuri katika Michezo ya Ligi Kuu Tanzania iliyosalia msimu huu, ili kufanikisha lengo la kuiweka salama timu hiyo ya mkoani Kagera.

Kagera Sugar ilipoteza mchezo uliopita dhidi ya Young Africans kwa kufungwa 5-0, juma lililopita katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es salaam.

Maxime amesema kuwa wanatambua walikwama kushinda mchezo uliopita jambo linalowapa nguvu kujipanga kwa michezo inayofuata, hivyo ametoa tahadhari kwa timu ambazo zinajiandaa kukutana na kikosi chake.

“Hatukuwa na siku nzuri dhidi ya Young Africans, ule ulikuwa mtego kwetu nasi tukaingia hivyo kwa sasa ambacho tunakifanya ni kujipanga kuwa imara kwa mechi zinazofuata.”

“Hakuna namna bado wachezaji wana juhudi na uwezo wao ni mkubwa, ndio maana wanashiriki ligi kwa makosa waliyofanya tutafanyia kazi ili tupate matokeo kwani mpira ni mbinu na wakati mwingine huwa unakuwa na matokeo tofauti,” amesema

Kagera Sugar inatarajia kukutana na Mbeya City Mchezo Aprili 23 dhidi ya Mbeya City, katika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba mkoani Kagera.

Kylian Mbappe aweka rekodi Paris Saint-Germain
Frank Lampard achimba mkwara Chelsea