Aliyewahi kuwa mlinda mlango wa klabu nguli za Ligi Kuu Tanzania Bara Simba SC, Young Africans na Azam FC Deogratius Munish ‘Dida’ huenda akajiungana klabu ya Ihefu FC inayoshiriki Ligi Kuu kwa mara ya kwanza msimu huu 2020/21.

Dida ambaye msimu uliopita aliitumikia Lipuli FC ya Iringa, hakufanikiwa kupata timu mwanzoni mwa msimu huu, hali iliyomlazimu kusubiri hadi dirisha dogo la usajili ambalo rasmi limefunguliwa leo Jumatano (Desemba 16).

Taarifa zinaeleza kuwa, mlinda mlango huyo atajiunga na Ihefu FC inayonolewa na kocha mzawa Zubeir Katwila kama mchezaji huru, na anatarajiwa kupelekea changamoto mpya kwenye lango la klabu hiyo.

Mbali na mlinda huyo kutajwa kuwa kwenye mipango ya kujiunga na Ihefu FC, pia uongozi wa klabu hiyo ya mkoani Mbeya umejipanga kusawajili kwa mkopo baadhi ya wachezaji kutoka kwenye klabu za Simba, Young Africans na Azam FC.

Tetesi zinaeleza kuwa wachezaji  hao ni Juma Mahadhi (Young Africans),  Miraji Athumani, Charles Ilanfya, Ibrahim Ame (Simba SC) na Andrew Simchimba (Azam FC).

Silinde asisitiza usimamizi miradi ya maendeleo
EU yatoa msaada kwa Tanzania bilioni 84