Kocha Mkuu wa Young Africans Cedrick Kaze amelazimika kuwapumzisha kwa muda baadhi ya wachezaji wake, baada ya kuonesha utovu wa nidhamu saa chache kabla ya kuanza kwa kambi ya vinara hao wa Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Kaze amechukua maamuzi hayo, kufuatia baadhi ya wachezaji hao kukaidi maagizo ya kufika kambini kwa wakati, baada ya mapumziko ya siku 10, ambazo zilikwisha rasmi jana.
Wachezaji wote wa Young Africans ambao walipaswa kufika kambini Kigambini Dar es salaam, walitakiwa kufanya hivyo kabla saa 6:30, lakini badhi yao walishindwa kwenda na muda huo maaluma mbao ulitarajiwa kupewa heshima na kila mmoja kikosini.
Wakati wachezaji wakiwasili baadhi ya wachezaji wakakutana na balaa jipya la kuzuiwa kuingia kambini baada ya kufika dakika tano baada ya muda uliopangwa.
Mastaa hao ni kiungo Haruna Niyonzima, Carlos Carinhos, Mukoko Tonomba na kipa Farouk Shikhalo huku mchezaji pekee aliyechelewa na kuruhusiwa kuingia ni beki wao mpya Dickson Job ambaye jana aliwasili kambini hapo kuanza kazi na alikuwa haelewi taratibu za Kaze.
“Wamerudishwa unajua kocha hataki masihala na muda na hajali jina lako na wameambiwa …