Baada ya sare ya nne dhidi Kagera Sugar katika mchezo wa ligi, Kocha Mkuu wa KMC FC Abdihamid Moalin, ameweka wazi changamoto zilizowafanya waruhusu mabao mengi ikiwemo kumkosa Mlinda Lango aliyepata majeruhi ya bega.

Mpaka sasa imecheza mechi 10 huku msimu uliopita katika idadi hiyo ilishika nafasi ya nane na kuruhusu mabao tisa katika mechi tatu, na kupata sare michezo minne na kushinda mitatu sawa na mabao sita.

Msimu huu kati mechi 10, KMC FC imeruhusu mabao 13 katika michezo mitatu na sare mechi nne na kushinda michezo mitatu ikiwa ni jumla ya mabao matano.

Licha ya Kocha huyo kumzungumzia Mlinda Lango amesema yapo mnaeneo mengi ya kuboresha; “Safu ya ulinzi na washambuliaji inahitaji marekebisho makubwa na siwezi kusema kama tutaongeza mchezaji yoyote ila mpaka kufikia nusu msimu malengo yangu ni kusalia katika nafasi isiyopungua ya tano au sita katika ligi.”

“Kuwa chini ya timu kama Simba SC, Young Africans na Azam FC sio jambo rahisi na ninawapongeza wachezaji wangu ijapo makosa yapo ila muda wa kuyarekebisha ni mkubwa hivyo hakuna kitakachoharibika.” amesema

“Maboresho ninayotaka kuyafanya kwa wachezaji wangu sio tu kwa ajili ya KMC FC bali hata kwa timu ya Taita na ni matamanio yangu wachezaji wangu watapata fursa.

Milioni 17 za GGML kung'arisha ATF Marathon 
Mila potofu chanzo ukatili wa kijinsia