Beki wa kushoto Liverpool, Andy Robertson amefanyiwa upasuaji wa wa bega baada ya kupata majeraha wakati akitumikia timu yake ya taifa ya Scotland.

Staa huyo alipata majeraha wakati akipambana kuwania mpira na kipa wa Hispania, Unai Simon timu hizo zilipokutana katika mchezo wa kufuzu michuano ya Euro 2024, hivi karibuni.

Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp amethibitisha Robertson amefanyiwa upasuaji na umekwenda vizuri.

“Tayari ameshafanyiwa upasuaji wa bega na umekwenda vizuri, hali yake inaendelea kuimarika taratibu.

“Bado haijafahamika kwamba atakaa nje ya dimba kwa muda gani hadi pale tutakapopata ripoti ya madaktari ambayo itatoka wakati wowote kuanzia sasa,” alisema Kocha Klopp.

Robertson, amecheza katika mechi nane za Ligi Kuu ya England msimu huu na kufunga bao moja, mechi iliyopita dhidi ya Everton, nafasi yake ilichukuliwa na Kostas Tsimikas.

Tsimikas mwenye umri wa miaka 27, pia alianza katika mechi ya Europa dhidi ya LASK Linz na Union Saint-Gilloise mechi ya Kombe la Ligi ya raundi ya tatu ilipocheza na Leicester City huku akianzia benchi mchezo wa Ligi Kuu ya England walipoikabili Bournemouth.

Klopp awali alishasema beki Joe Gomez ambaye hucheza beki wa kati au kulia au kinda Luke Chambers wanaweza kuwa mbadala kama wakihitajika.

Kibu Denis afanywa mfano Simba SC
Ibrahim Class, Majiha kupanda ulingoni