Aliyekuwa Kocha Msaidizi wa Young Africans Riedoh Berdien ameiitahadharisha Klabu hiyo ya Jangwani kuelekea mchezo wa Mkondo wa Kwanza wa Nusu Fainali, Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya Marumo Gallants.

Young Africans itaanzia nyumbani keshokutwa Jumatano (Mei 10) katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, kisha itaifuata Marumo Gallants Afrika Kusini kwa mchezo wa Mkondo wa Pili utakaopigwa Mei 17.

Berdien ambaye kwa sasa ni Kocha wa viungo wa kikosi cha Mabingwa wa Afrika Kusini amesema Young Africans wanapaswa kuwa makini wakati wote endapo wanahitaji kutinga Fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika msimu huu 2022/23.

 Mamelod Sundowns, amekiri kuwatazama Marumo Gallants na  kuwaonya Yanga kuwa wanapaswa kucheza kwa tahadhari kubwa kama wanataka kutinga Fainali.

Amesema ameifuatilia Marumo kwa muda mrefu katika michezo ya ndani na nje ya Afrika Kusini na amebaini timu hiyo ina mbinu za ajabu licha ya kusuasua katika Ligi Kuu ya DSTV.

Kocha Riedoh amesema: “Marumo ni miongoni mwa timu zinazofanya vizuri ndani ya ligi ya Afrika Kusini.”

“Licha ya kuwa ni timu changa sana lakini wamefanya uwekezaji mkubwa kuhakikisha wanakuwa na kikosi cha ushindani.”

“Hii ni mara yao ya kwanza wanashiriki mashindano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika na unaweza kuona wamefanikiwa kufuzu hatua ya Nusu Fainali, hii inatosha kueleza ni kwa kiasi gani wana mipango mizuri.”

Ni kweli Young Africans kwa sasa wanaonekana kuwa na kiwango bora lakini ni lazima wacheze kwa tahadhari kubwa michezo yote miwili kama wanataka kufuzu hatu ya Fainali.”

Marumo Gallant ilifanikiwa kufika Nusu Fainali Kombe la Shirikisho Barani Afrika kwa ushindi wa jumla wa 2-1 dhidi ya Pyramid ya Misri, huku Young Africans ikiibamiza Rivers United ya Nigeria kwa ushindi wa jumla wa 2-0.

Mashabiki Liverpool wazomea wimbo wa taifa
Tekelezeni majukumu kwa manufaa ya Taifa - Dkt. Luhende