Kocha Mkuu wa Coastal Union Juma Mgunda amesema wanawaheshimu wapinzani wao Young Africans, huku kikois chake kikiwa tayari kwa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaochezwa baadae Uwanja wa CCM MKwakwani, Jijini Tanga.

Mgunda amtoa kauli hiyo baada ya kukamilisha maandalizi ya kikosi chake, ambacho leo Alhamis kitakua nyumbani, huku mashabiki wake wakiwa  na matumaini makubwa ya kuwasimamisha Young Africans ambao hawajapoteza mchezo wa Ligi Kuu msimu huu.

Mgunda amesema anatarajia Young Africans watapambana kama itakavyokua kwa wachezaji wake, lakini bado naamini msema kweli atakua dakika 90 za mchezo wa leo.

“Tunawahesimu Yanga kabisa kwa kuwa tunajua kwamba wanaongoza ligi, ikiwa mpinzani wako lazima umheshimu hilo lipo wazi.”

“Muhimu ndani ya uwanja kucheza fair play hilo la kwanza na pili tupo kwenye ushindani hii ni ligi nasi pia tupo kwenye ushindani muhimu kila mmoja kulitambua hilo.”

“Wachezaji wangu wote wapo vizuri kuanzia kwenye mazoezi ya mwisho mpaka morali yao hivyo kikubwa ni kusubiri na kuona. Mashabiki wajitokeze kwa wingi uwanjani kushuhudia ushindani utakavyokuwa.” Amesema Mgunda.

Timu zote mbili zimecheza jumla ya michezo 21 msimu huu 2020/21 ndani ya ligi.

Timu hizo zilipokutana kwenye mzunguko wa kwanza Uwanja wa Benjamin Mkapa Young Africans ilishinda mabao 3-0, ambapo ulikuwa ni mchezo wa mwisho kwa Kocha Zlatko Krmpotic aliyefutwa kazi mazima.

Kwa sasa kikosi cha Young Africans kipo chini ya Kocha Cedric Kaze ambaye anakutana ndani ya uwanja na Juma Mgunda wa Coastal Union.

Coastal union inashika nafasi ya 13 na alama zake 23 inakutana na Young Africans iliyo nafasi ya kwanza na alama zake kibindoni ni 49.

Serengeti Boys safarini Morocco
Nchimbi na wenzake kuikosa Coastal Union