Kocha wa Hull City, Marco Silva amejiuzuru kuendelea kuitumikia klabu ya Hull City iliyoshuka daraja kwenye ligi kuu ya England msimu huu.
 
Silva ambaye ni raia wa Ureno alichukua mikoba ya timu hiyo toka kwa Mike Phelan mwezi Januari na jukumu lake lilikuwa ni kuisaidia timu hiyo isishuke daraja.
 
Meneja huyo wa zamani wa Sporting Lisbon na Olympiakos anahusishwa na mpango wa kwenda kujiunga na timu ya Watford ambayo imemtimua mkufunzi wake wa kiitaliano Walter Mazzarri.
 
Hata hivyo, mbali na Silva makocha wengine pia wamejiondoa kwenye timu hiyo ambao ni kocha msaidizi Joao Pedro Sousa,kocha wa kikosi cha kwanza Goncalo Pedro pamoja na kocha wa makipa Hugo Oliveira

Video: Chenge, Werema wajivua lawama, Acacia waomba tume huru, uchunguzi mpya
Magazeti ya Tanzania leo Mei 27, 2017