Kocha Mkuu wa Namungo FC Hemed Suleyman Morroco anakabiliwa na mtihani mkubwa leo Alhamis (Desemba 02), na kama atafeli ataondoka na kwenda kusaka rizki mahala pengine.

Morroco anakabiliwa mtihani wa kuhakikisha kikosi chake hakipotezi mchezo wa Mzunguuko wasaba wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Ruvu Shooting ambao watakua nyumbani Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani.

Tayari Kocha huyo kutoka Zanzibar ameshapewa taarifa na Kamati ya Utendaji ya Namungo FC chini ya Mwenyekiti wake Hassan Zidadu, akitakiwa kupata matokeo chanya kwenye mchezo wa leo, na kama atashindwa safari itamuhusu.

Mbali na Kocha Morocco, taarifa hiyo inamuhusu Afisa Mtendaji Mkuu wa Namungo FC Omary Kaaya ambaye ana jukumu la kuhakikisha shughuli za kila siku za klabu hiyo zinakwenda vizuri.

Namungo FC imekua na wakati mgumu wa kupata matokeo katika michezo ya Ligi Kuu Msimu huu, kwani michezo uliopita ilipoteza kwa kufungwa mabao 3-1 dhidi ya Tanzania Prisons, kabla ya hapo ilipata sare ya 1-1 dhidi ya Young Africans huku Simba SC ikiichapa bao 1-0 Uwanja wa Benjimin Mkapa jijini Dar es salaam.

WHO yatoa onyo
Edo Kumwembe amsambaza Martin Saanya