Nahodha na Mshambuliaji wa zamani wa Timu ya Taifa ya Ivory Coast Didier Drogba ametangazwa kuwa Kocha Mkuu wa timu ya taifa hilo kwa mkataba wa miaka minne.
Hii ni mara ya kwanza kwa mchezaji huyo wa zamani wa taifa hilo kupata wadhifa wa kuwa kocha mkuu baada ya kumaliza mafunzo ya ukocha ambapo ana leseni ya UEFA PRO.
Aidha inaelezwa kuwa Drogba amemuomba Yaya Toure kuungana nae kama kocha msaidizi na anasubiri majibu kutoka kwa mchezaji huyo mwenzake wa zamani.
Drogba amepewa vipaumbele vya shirikisho kumpa wadhifa huo ni kushinda kombe la mataifa ya Afrika 2024 na 2025 na kuhakikisha anaiongoza Ivory coast kushinda taji la kombe la dunia 2026.