Baada ya kuambulia alama moja dhidiya Simba SC, Kocha Mkuu Young Africans Nasreddine Nabi amekosoa mfumo wa mpinzani wake Franco Pablo Martin kwa kusema unatofauti kubwa na ule uliokuwa ukitumika na kocha aliyepita Didier Gomes.

Nabi amesema kuwa kuna tofauti kubwa ya uchezaji ambao upo ndani ya Simba kwa wakati huu baada ya kupata kocha mpya ambaye ni Franco.

Kocha huyo kutoka nchini Tunisia amesema: “Kuna mabadiliko kwenye upande wa uchezaji unaona kwamba kwa sasa kocha huyu (Franco) anapenda kujilinda tofauti na aliyepita, (Gomes) ambaye alikuwa anapenda kushambulia muda mwingi,”

Gomes aliomba kuondoka Simba SC Oktoba 26 baada ya timu hiyo kutokewa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kufungwa mabao 3-1 dhidi ya Jwaneng Galaxy, Uwanja wa Mkapa.

Kwa sasa mikoba yake ipo mikononi mwa Franco ambaye alikiongoza kikosi hicho kwa mara ya kwanza kwenye Kariakoo Dabi mbele ya Young Africans na kutoshana nguvu bila kufungana Jumamosi (Desemba 11).

Salum Mayanga akabidhiwa Mtibwa Sugar
Rais Samia : Madini kuongezwa thamani nchini