Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans Nasreddine Nabi amesema iwe isiwe safari hii hatokubali kikosi chake kushindwa Kimataifa.

Young Africans itacheza mchezo wa Mkondo wa Kwanza Hatua ya Mtoano Kombe la Shirikisho Barani Afrika, dhidi ya Club Africain ya Tunisia kesho Jumatano (Novemba 02) katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Kocha Nabi amesema ameshajifunza kutokana na makosa walioyafanya kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Al Hilal ya Sudan, ambapo kikosi chake kilishindwa kupata ushindi nyumbani Dar es salaam.

Amesema dawa ya kufanikisha mpango huo ni kusaka ushindi wa zaidi ya mabao 2-0 katika Uwanja wa nyumbani, ili iwe rahisi kwao watakapokwenda Uwanja wa ugenini.

“Ki ukweli kutolewa katika hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika kumenipa funzo mimi pamoja na wachezaji wangu, bila ya kusahau viongozi wetu.”

“Ki ukweli katika Ligi ya Mabingwa Afrika tulishindwa kufanya vizuri kwa kukosa matokeo mazuri nyumbani. Ninaamini tungepata ushindi wa mabao zaidi mawili, basi tungevuka hatua inayofuata.”

“Hivyo basi safari hii tumejipanga kupata matokeo bora mchezo huu wa kwanza ili kujihakikishia nafasi ya kumaliza kazi tutakapocheza ugenini.” amesema Nabi

Baada ya mchezo wa kesho Jumatano (Novemba 02) Young Africans itakwenda ugenini Tunis-Tunisia kucheza mchezo wa Mkondo wa Pili utakaopigwa Uwanja wa Olympique de Radès, Novemba 09.

Nelson Okwa yamkuta mengine Simba SC
Shomari Kapombe arudisha fadhila Simba SC