Kocha wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC Franco Pablo Martin amelalamikia ratiba ya Ligi Kuu kwa kusema imewabana, hali ambayo inamuuwia vigumu kukiandaa kikosi chake.

Simba SC leo Alhamis (april 07) inacheza dhidi ya Coastal Union, Uwanja wa CCM Mkwakwani Jijini Tanga na kisha itasafiri hadi mkoani Kilimanjaro Kupapatuana na Polisi Tanzania Jumapili (April 10), Uwanja wa Ushirika.

Kocha Pablo amesema: “Tumekuwa na michezo inayofuatana na tulifanya mazoezi kabla hatujasafiri, sijui utakuwa ni mchezo wa namna gani lakini lengo letu ni kupata ushindi.”

Mbali na mchezo dhidi ya Polisi Tanzania, April 13 Simba SC itacheza Robo Fainali Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’ dhidi ya dhidi ya Pamba FC ya Mwanza.

Baada ya mchezo huo Mabingwa hao watetezi wataingia kwenye mpango wa kuiwakilisha Tanzania Kimataifa kucheza Robo Fainali Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini, April 17 Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

April 22-24 Simba SC itacheza mchezo wa Mkondo wa pili Robo Fainali Kombe la Shirikisho Barani Afrika ugenini Afrika Kusini dhidi ya Orlando Pirates.

Mabinti wa Putin wawekewa vikwazo Marekani
Agrey Morris afunguka vita yake na Mayele