Baada ya kutinga Raundi ya Kwanza ya mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kuing’oa African Stars ya Namibia kwa faida ya bao la ugenini na kutambua sasa itavaana na Simba SC, Kocha Mkuu wa Power Dynamos ya Zambia, Mwenya Chipepo ameonekana kuingiwa ubaridi akisema anawafahamu vizuri wapinzani wao ili na sasa wanajipanga upya kuvunja rekodi ya Wekundu hao.

Dynamos imetinga hatua hiyo baada ya awali kufungwa 2-1 ugenini kisha jumamozi (Agosti 26) ikalipa kisasi nyumbani kwa kushinda 1-0 na kufanya matokeo ya mwisho kuwa 2-2 na kupenya kwa kanuni ya faida ya bao la ugenini na itavaana na Simba SC mwezi ujao ikiwa ni mwezi mmoja tangu zikutane kwenye pambano la kirafiki la kimataifa kwenye Tamasha la Simba Day na miamba hiyo ya Zambia kulala 2-0 Kwa Mkapa.

Akizungumza kutoka nchini Zambia, Chipepo alisema sio wageni kwa Simba SC, wanaifahamu vizuri kuanzia ubora wao wa timu na rekodi zao kwenye michuano hiyo, hivyo wanajipanga ili kuivunja, kwani kwa miaka ya hivi karibuni, Simba SC imekuwa ikifuzu makundi na kukwamia Robo Fainali ya Michuano ya CAF.

Simba SC ni timu nzuri na ina wachezaji wengi wenye zoefu, tumecheza nao mechi ya kirafiki Agosti 6 mwaka huu tukafungwa mabao 2-0, kilikuwa ni kipimo sahihi kwetu tumesawazisha makosa na kufanikiwa kutinga hatua ya kwanza,” amesema Chipepo na kuongeza

“Kukutana nao sio habari mpya kwetu tulitarajia kitu hiki tutaingia kwa kuwaheshinu kutokana na rekodi yao nzuri dhidi yetu na ubora wao kwenye michuano hii, malengo yetu ni kutinga hatua ya makundi tutapambana kuhakikisha lengo hilo linatimia.”

Chipepo amesema wanafahamu ubora wa kikosi cha Simba SC ulipo na udhaifu wao hivyo watapambana kuhakikisha wanafanya jitihadi za kuwadhibiti ili waweze kuweka heshima katika mechi za mashindano.#

Akizungumzia ubora wa mchezaji mmoja mmoja ndani ya kikosi cha Simba SC amesema kila mchezaji aliye ndani ya kikosi cha timu hiyo ni bora na ndio maana kasajiliwa, hivyo hawezi kuzungumzia mchezaji mmoja mmoja.

“Naheshimu kila mchezaji na wachezaji wangu mara baada ya kutinga hatua inayofuata tulikaa pamoja na kukumbushana aina ya timu tunayoenda kukutana nayo.”

Tabasamu la utalii wa Aikolojia laonekana Singida
Wananchi wapewe elimu ya Katiba: Dkt. Ndumbaro