Mshambuliaji wa klabu ya Tottenham Hotspur Erik Lamela ameitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Argentina, kitakachoingia kambini juma lijalo kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Mexico.
Lamela, ambaye tayari ameshaitumikia timu ya taifa ya Argentina mara 23, kwa mara ya mwisho alicheza mchezo wa kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia 2018, dhidi ya Venezuela mwaka 2016, lakini aliachwa kwenye kikois kilichokwenda nchini Urusi, kufuatia kuwa majeraha.
Kocha wa muda wa kikosi cha Argentina Lionel Scaloni, pia amemuita kiungo wa klabu ya Racing Club mwenye umri wa miaka 20 Matias Zaracho.
Bado mawazo na mapendekezo ya mshambuliaji na nahodha Lionel Messi, ya kutotaka kuitwa kwenye kikosi cha Argentina yanaendelea kuheshimiwa hadi mwaka 2019, ambapo alitaka iwe hivyo kwa kuhitaji muda wa kupumzika, baada ya Argentina kushindwa kufanya vyema kwenye fainali za kombe la dunia.
Kikosi cha Argentina kitacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Mexico katika mji wa Cordoba Novemba 16.
Kikosi kamili kilichotajwa na kocha Scaloni.