Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Soka Afrika Mashariki na Kati kwa Wanawake ‘Simba Queens’ Charles Lukula, amewatoa hofu Mashabiki kwa kusema kikosi chake kipo tayari kwa Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Simba Queens itaanza Kampeni ya kusaka taji la Afrika Oktoba 30 kwa kucheza na wenyeji AS FAR (Morocco), kwenye Uwanja wa Moulay Hassan, mjini Rabat.
Akizungumza katika Mkutano na Waandishi wa Habari Kocha Charles Lukula, amesema amekiandaa vizuri kikosi chake kuelekea kwenye Michuano hiyo, sambamba na kucheza michezo ya Kirafiki ambayo imekua kipimo kizuri kwa wachezaji.
“Hatuna majeruhi hata mmoja, tunaenda Morocco tukiwa na kikosi kamili. Tumecheza mechi za kirafiki na timu ipo kwenye hali nzuri ya ushindani.” amesema Charles Lukula ambaye alikiongoza kikosi cha She Coperates ya Uganda wakati wa Michuano ya Afrika Mashariki na Kati ‘CECAFA’ iliyofanyika jijini Dar es salaam mwezi Agosti
Katika Michuano ya Klabu Bingwa Afrika kwa Wanawake Simba Queens imepangwa ‘Kundi A’ na wenyeji AS FAR (Morocco), Green Buffaloes (Zambia) na Determine Girls (Liberia).
Simba Queens itaanza Kampeni ya kusaka taji la Afrika Oktoba 30 kwa kucheza na wenyeji AS FAR (Morocco), kwenye Uwanja wa Moulay Hassan, mjini Rabat.
Mabingwa Watetezi Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini) wamepangwa ‘Kundi B’ sambasamba na timu za Bayelsa Queens (Nigeria), Wadi Degla (Misri) na TP Mazembe (DR Congo).