Kocha Mkuu wa KMC FC Hitimana Thierry amepania kuharibu Rekodi ya Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans ya kutofungwa michezo 43 mfululizo tangu msimu uliopita 2021/22.
Kocha Hitimana ambaye aliwahi kupita Simba SC kabla ya kutimkia KMC FC amesema, amejipanga kuitibulia Young Africans kupitia mchezo wa kesho Jumatano (Oktoba 26), utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.
Hitimana amesema amekiandaa vizuri kikosi chake kwa ajili ya kuikabili Young Africans, ambayo amekiri ameifuatilia na kujua wapi ulipo udhaifu wake ambao atautumia kupata alama tatu.
Wakati huo huo Afisa Habari na Mashabiki wa KC FC Christina Mwagala amesema: “Tunakwenda kuivunja Rekodi ya hiyo kwa kuwa tuna vijana ambao wanajua nini timu inahitaji, Young Africans inakwenda kupasuka na ninasema hivyo kwa kuwa tunajua mipango yote.”
“Ninachowaambia mashabiki wa Young Africans wake kwa wingi ili walie vizuri na timu yao, kwa kuwa PIRA MAPATO na PIRA KODI ndiyo staili ambayo tunakwenda kuwapigia.”
KMC FC inakwendea kucheza na Young Africans katika Uwanja wa ugenini, huku ikiwa na kumbukumbu ya Ushindi wa 2-1 dhidi ya Azam FC, huku Young Africans ikikumbukia sare ya 1-1 dhidi ya Simba SC.