Kocha mkuu wa Simba Patrick Aussems raia wa Ubelgij amesema kuwa wanatambua uwezo wa kikosi cha Mtibwa Sugar  kutokana na ubora ila wao lengo lao ni  kupata ushindi mbele ya wapinzani wao.

Aussems amesema kuwa maandalizi ya kikosi yapo vizuri na kila mchezaji anajua jukumu lake la kufanya kuelekea mchezo wao dhidi ya Mtibwa Sugar.

Simba itashuka uwanja wa Uhuru Septemba 13 kuminyana na Mtibwa Sugar ikiwa ni mchezo wake wa pili wa ligi baada ya ule wa kwanza kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 mbele ya JKT Tanzania.

“Tunahitaji kufanya vizuri na kupata matokeo mbele ya Mtibwa Sugar, kikubwa ambacho kwa sasa tunakifanya ni kumalizia maandalizi ya mwisho kabla ya kukutana nao uwanjani.

“Ushindani ni mkubwa kwani kila timu inahitaji ushindi tumejipanga kufanya vema sapoti tunahitaji kutoka kwa mashabiki,” amesema.

Simba ni mabingwa watetezi wa ligi, mchezo wao wa mwisho msimu uliopita walishinda kwa idadi ya mabao 3-0 mbele ya Mtibwa uwanja wa Uhuru leo wamefanya mazoezi viwanja vya Gymkyana.

Mtibwa Sugar yaapa kuifunga Simba
Vincent Kompany aandaliwa mechi ya kuagwa