Kocha Mkuu wa Singida Fountain Gate FC Hans van der Pluijm amekiri kufurahishwa na kiwango kilichooneshwa na wachezaji wake kwenye mchezo wa kirafiki waloucheza juzi Jumatatu (Julai 24) dhidi ya Namungo FC na kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Akizungumzia akiwa kambini mjini kAratu mkoani Arusha Kocha Mkuu wa Singida Fountain Gate, Hans van Pluijm, amesema wachezaji wake wameonesha kile anachokihitaji na kudai wameanza kuwa na muunganiko mzuri.

“Ninawapongeza wachezaji wangu wamefuata maelekezo niliyowapa tumefanikiwa kutoka na ushindi, hii ni ishara nzuri kuelekea mchezo wetu wa Ngao ya Jamii utakaotukutanisha na timu ya Simba SC,” amesema Pluijm.

Amesema mchezo ulikuwa mgumu na wenye upinzani mkubwa kwani kila timu ilicheza vizuri kutokana na usajili zilizofanya.

Kwa upande wa Msemaji wa timu hiyo, Hussein Masanza, amesema maandalizi kuelekea Siku ya Singida (Singida Big Day), inayotarajiwa kufanyika Agosti 2, mwaka huu, yanaendelea vema na kwamba wataitumia siku hiyo kutangaza wachezaji wao ambao wamewasajili msimu huu.

Afrika inakabiliwa na changamoto - Rais Samia
Gavana Kortini kwa kumiliki Silaha kinyume cha sheria