Kocha Msaidizi wa Singida Fountain Gate, Thabo Senong amesemna Ligi Kuu Tanzania Bara bado ni ngumu na haitabiriki kwa sababu kila timu inakuja tofauti katika mchezo husika.
Thabo amesema hayo baada ya kushinda 3-1 dhidi ya Mashujaa juzi Jumatatu (Novemba 06) katika Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma.
Kocha huyo amesema matokeo hayo bado hayawaaminishi wanaweza kuchukua alama tatu katika mechi zijazo kama tu hawatozidi kujiimarisha na kupunguza makosa.
“Kuna makosa ambayo tuliyafanya katika mechi na Ihefu sasa yale ndio tunatakiwa kuyapunguza kwa kiasi kikubwa, ligi haitabiriki na kila timu imejiandaa kushinda mechi zake.”
Akizungumzia mchezo wao dhidi ya Mashujaa alisema; “Mashujaa ni timu nzuri sana na ilitupa changamoto kubwa ndani ya uwanja, tulitengeneza nafasi nyingi na wenzetu walifanya hivyo pia, lakini sisi tumeshinda.”
Matokeo hayo yanaifanya Singida FG kutoka nafasi ya nane hadi nane ikiwa na pointi ll. Singida imecheza mechi tisa, imeshinda tatu, sare tatu, imefungwa tatu huku ikiruhusu mabao 11 na kufunga 11.