Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Nigeria (Super of Eagles), Gernot Rohr amesema golikipa wa muda mrefu wa timu hiyo, Vincent Enyeama atarudi kikosini pindi atakapo kuwa katika hali nzuri.
Mwaka 2015, Enyeama ambaye kwa sasa ametemwa na club yake ya Lille ya Ufaransa, alitangaza kustaafu kuichezea timu ya taifa ikiwa ni siku moja baada ya kupokonywa nafasi ya ukampteni wa timu hiyo na kuripotiwa kuwepo msuguano kati yake na aliyekuwa kocha wa Super Eagles, Sunday Oliseh.
Katika mahojiano aliyoyafanya hivi karibuni, kocha mpya wa kikosi hicho Rohr amesema amekuwa akizungumza na Enyiama ili aweze kurejea kuichezea timu ya Taifa.
- Andre Schurrle Hadi Mwezi Septemba
- McGregor atamba ‘atakavyompasua’ Mayweather ndani ya raundi mbili
“Ukweli ni kwamba nina mahusiano mazuri na Enyeama. Nilipompigia simu alinambia ana tatizo na chama cha soka cha Taifa, akanambia ‘siwezi kujiunga na timu kwa wakati huu’,’’ amesema Rohr.
Kocha huyo ameongeza kuwa ameendelea kuwasialiana na Enyaama ambaye amemueleza hivi sasa ni majereruhi na ameonesha nia ya kurudi kuichezea timu ya taifa atakapokuwa buheri wa afya.