Wakati kikosi cha mabingwa Tanzania Bara Simba SC, kikianza maandalizi ya kuelekea mchezo wa mzunguuko watatu wa Ligi Kuu dhidi ya Biashara United Mara, kocha mkuu Sven Vandenbroeck amesema anahitaji muda wa siku kadhaa ili kuirejesha timu yake kwenye kilele cha msimamo wa ligi hiyo.

Simba SC ina alama nne baada ya kushinda mchezo moja dhidi ya Ihefu FC na sare moja dhidi ya Mtibwa Sugar, matokeo ambayo yameiweka kwenye nafasi ya tano, ikitangulia nafasi moja dhidi ya Young Africans iliyo nafasi ya sita, baada ya kukamilika kwa mzunguko wa pili.

Kocha Sven amesema malengo yake makubwa ni kuona timu ya Simba inarejea hadhi yake ya kuongoza msimamo wa Ligi Kuu na kutwaa ubingwa wa Tanzania Bara kwa mara ya nne mfululizo.

Amesema amejipanga kuhakikisha hali hiyo inafanikiwa hadi kikosi chake kitakapokuwa kimeshashuka dimbani mara tano ama sita.

“Mipango tulionayo ni kuwa baada ya michezo kuanzia mitano ama sita tunataka kuona tunaongoza ligi.

“Tunajua haitakuwa rahisi lakini tutapambana kulifanikisha hilo, bila ya kujali aina ya matokeo ambayo tutayapata,” alimaliza Sven.

Timu ya Simba SC leo Jumanne Septemba 15, imeanza maandalizi ya mchezo wa mzunguuko wa tatu wa Ligi Kuu dhidi ya Biashara United Mara utakaopigwa Uwanja wa Mkapa, Septemba 20 na utakuwa mchezo wa kwanza ndani ya ardhi ya Da es salam kwa wekundu hao kwa msimu huu 2020/21.

Sevilla CF yamnasa Marcos Javier Acuña
Azam FC yatangaza hatari Ligi Kuu