Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Tanzania Bara (VPL) na Kombe la Shirikisho (ASFC) Simba SC Sven Vandenbroeck, ameahidi burudani zaidi, baada ya kikosi chake kufanya hivyo wakati wa mchezo wa mzunguuko watatu wa Ligi Kuu dhidi ya Biashara United Mara waliokubali kibano cha mabao manne kwa sifuri Jumapili, Septemba 20.

Kocha Sven amesema kikosi chake kimetangaza vita kwa mpinzani wao anayefuata (Gwambina FC), na kusema wachezaji wake wamejipanga kuonyesha kiwango cha juu zaidi ya walichoonyesha katika mchezo uliopita.

Kocha huyo kutokanchini Ubelgiji amesema, wachezaji wake hasa wa kigeni wameonyesha kiwango kizuri na matumaini yake wataimarika zaidi na kuipa timu hiyo matokeo mazuri kwenye mchezo huo utakaochezwa Jumamosi, Septemba 26 usiku.

Ameongeza mbali na kucheza kwa kiwango kizuri na kuifunga Biashara United Mara FC, kuna mapungufu madogo aliyaona na atayafanyia kazi kabla ya kukutana na Gwambina FC ili wapate kile wanachokihitaji.

“Nimeridhishwa na kiwango kizuri walichokionyesha wachezaji wangu, natarajia hata mechi ijayo watacheza kiwango kizuri kama leo (juzi), au zaidi hasa ukizingatia tunacheza tena kwenye uwanja wa nyumbani,” amesema Sven.

Ameeleza malengo yao ni kuendelea kupata ushindi katika kila mchezo na kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kutetea taji la Ligi Kuu Bara na kujiweka tayari na michuano ya kimataifa.

“Malengo yetu ni kuhakikisha tunatetea taji letu, tunahitaji kupambana ili kupata matokeo chanya katika kila mechi, hatutaidharau timu yoyote tutakayokutana nayo, kwa sababu ligi ni ngumu na imekuwa na ushindani mkubwa,” amesema Sven.

Baada wa ushindi wa manne kwa sifuri Simba SC imefikisha alama saba na inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu, sawa na Young Africans na Dodoma Jiji FC lakini tofauti ya mabao yakufunga na kufungwa yanawabeba mabingwa hao wa VPL mara tatu mfululizo.

Uchambuzi :Ushauri wa Jaji Maraga kwa Rais Kenyatta.
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Septemba 22, 2020