Baada ya Tanzania Prisons kushinda michezo mitatu mfululizo na kukaa katika nafasi nzuri katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Kocha Mohamed Abdallah Bares, amepania kukiongoza vyema kikosi chake kufanya vizuri zaidi katika michezo iliyosalia.

Tanzania Prisons inashika nafasi ya tisa katika msimamo baada ya kuvuna alama 31 katika michezo 27 iliyocheza hadi sasa.

Katika michezo mitatu mfululizo iliyopita, ilipata ushindi dhidi ya Namungo (3-2), Ruvu Shooting (3-1) na Geita Gold (3-1).

Akizungumza baada ya kuiongoza timu yake kuichapa Geita Gold mabao 3-0, Bares alisema pamoja na mechi za lala salama kuwa na ushindani mkubwa, amepanga kuiongoza timu yake kupata matokeo mazuri ambayo yatazidi kuiepusha timu kujiweka katika nafasi nzuri ya kubaki Ligi Kuu.

“Katika kupambania michezo iliyobaki, kila timu inahitaji kujinasua kushuka daraja, kwa kucheza kwa nguvu na maarifa kwenye michezo iliyobaki hivyo huu ni wakati wa kuzidi kukiimarisha kikosi changu na kuendelea kufanya vyema,” alisisitiza.

Kikosi hicho kimebakiza michezo dhidi ya Kagera Sugar, KMC na Young Africans.

Raphael Varane amfikirisha Erik ten Hag
Uholanzi yaridhishwa mazingira, Demokrasia utawala bora