Kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Wales, Rob Howley amerudishwa nyumbani kutoka katika kambi ilipokuwa timu yake ikijiandaa na michuano ya Kombe la Dunia ya ‘Rugby Union’ kwa tuhuma za kujihusisha na mchezo wa kubashiri (bettting).
Baada ya kugundulika kuwa kocha huyo alibashiri mechi za Rugby Union amesimamishwa kujihusisha na masuala yoyote ya mchezo wa Rugby, na atakumbana na adhabu ya kufungiwa kwa kukiuka kanuni ambapo haziruhusu wahusika wa michezo (wachezaji, makocha na viongozi) kushiriki kubeti kwani wanaweza kupelekea kupanga matokeo.
Kocha huyo raia wa Uingereza ameondolewa katika kambi hiyo, zikiwa zimebakia siku sita tu kabla ya Wales kucheza mchezo wao wa kwanza dhidi ya Georgia katika michuano hiyo kombe la Dunia inayofanyika Japan.
Aidha, nafasi ya Rob Howley ambaye amejiunga na timu hiyo tangu mwaka 2008 imetangazwa kurithiwa na kocha Stephen John hadi 2020.