Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Brazil, Tite amejibu vijembe vya Rais wa Marekani, Donald Trump alivyovitoa kwa timu ya taifa ya nchi hiyo kwenye Ikulu yake ya ‘White House’
Mwezi uliopita, Rais wa shirikisho la soka duniani, Gianni Infantino alitembelea Ikulu ya Marekani, ndipo Rais Trump alipoonekana kuipiga vijembe timu ya Taifa ya Brazil kufuatia kutolewa kwake katika hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la dunia mwaka huu nchini Urusi.
Ameyasema hayo alipokuwa akijibu swali la mwanahabari mmoja wa Brazil katika ziara hiyo, ambapo Rais Trump alimpiga kijembe kwa kusema.
“Taifa la soka nafikiri mmepata tatizo hivi karibuni,”amesema Trump
Kwa upande wake Kocha wa Brazil alipoulizwa kuhusu kauli hiyo ya Rais Trump katika mkutano na wanahabari kuelekea mchezo wa kirafiki dhidi ya El Salvador utakaochezwa nchini Marekani, amesema kuwa jibu lake kwa Trump ni kwamba wameshinda kombe la dunia mara tano.
Brazil itacheza mchezo wake wa pili wa kirafiki dhidi ya El Salvador baada ya kuibuka na ushindi katika mchezo wa kwanza dhidi ya Marekani kwa mabao 2-0.
-
David Seaman amtaka Leno kustahamili
-
Icardi, Dybala kuongeza nguvu dhidi ya Colombia
-
Ivan Rakitic: Luka Modric mchezaji bora wa dunia
Katika mchezo huo dhidi ya Marekani, mshambuliaji tegemeo wa timu hiyo, Neymar Jr alikabidhiwa unahodha wa kudumu wa timu ya taifa ya Brazil ambapo alifunga bao lake la 58 kwenye timu hiyo linalomuweka nafasi ya tatu katika listi ya wafungaji bora wa muda wote wa nchi hiyo.