Uongozi wa Yanga kupitia kwa afisa habari wao Jerry Muro umetoa taarifa za msiba wa mama mkwe wa kocha msaidizi wa klabu ya Yanga Charles Boniface (mama mzazi wa mkewake Betty Mkwasa) na kocha huyo hajaungana na timu kusafiri kwenda Morogoro na badala yake yupo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya taratibu za kusafirisha mwili wa marehemu kuelekea Iringa.
“Mwalimu wetu mkwasa amefiwa na mama mkwe wake ambaye ni mama mzazi wa mke wake Bi. Betty Mkwasa. Tayari katibu mkuu wa Yanga Dr. Jonas Tiboroha ameungana na familia ya mwalimu wetu kwa ajili ya msiba wa mama mkwe wake ambao leo wanasafirisha kwenda Iringa kwa mazishi”, amesema Muro.
“Mara baada ya mazishi, ataungana na timu Morogoro kwa ajili ya mchezo wa Jumatano dhidi ya Mibwa Sugar”.
“Kwa wanachama wetu na wapenzi wa Yanga tuungane katika kipindi hiki kigumu cha mwalimu wetu kwa kuondokewa na mama mkwe wake”.
Mkwasa alikuwepo jana kwenye benchi la ufundi la kikosi cha Yanga akikiongoza kikosi hicho kuibuka na ushindi wa goli 2-0 dhidi ya watani wao wa jadi Simba SC kwenye mchezo wa raundi ya nne ya ligi kuu Tanzania bara uliochezwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Maftah Alaani Kwa Uchungu Kitendo Cha Juma Nyosso
Mourinho Aukosoa Mfumo Wa Newcastle Utd