Baada ya kushuhudia timu yake ikiambulia kipigo cha mabao 5-0 kutoka kwa Simba, Kocha wa timu ya Hard Rock, Muhibu Kanu amesema wachezaji wake walikuwa na hofu.

Kanu amesema mchezo huo umemsaidia kuona wapi ambapo kuna mapungufu katika kikosi chake, ambapo atayafanyia kazi lakini akadai kuwa wachezaji wake walikuwa na hofu kwa kuwa waliona wanacheza na timu kubwa.

Alidai kuwa ameona mapungufu na kwa kuwa ligi ya Zanzibar inatarajiwa kuanza hivi karibuni, anaamini Simba ilikuwa ni kipimo kizuri kwa wachezaji wake na benchi lao la ufundi limeshaona upungufu ulipo.

“Sijalia kufungwa kaisi kikubwa cha mabao, lakini naamini wachezaji wangu watakua wamejifunza kitu, na kwa upande wangu nimeona mapungufu yapo wapi, na ninaahidi nitayafanyia kazi ili kufanya maboresho.

“Wachezaji wangu walionyesha uoga dhidi ya wapinzani wao, na hii walijitengenezea mazingira ya kuogopa tangu mwanzo, kwa sababu ya jina la timu pinzani ya Simba, lakini bado hilo ni tatizo ambalo nimelibaini, nitalifanyia kazi ili kuwarejesha wachezaji katika saikolojia ya kupambana, na sio kuogopa jina”. Amesema Kanu

Mchezo wa jana ulikua wa kwanza kwa kocha Muhibu Kanu tangu alipomaliza masomo ya ukocha mkoani Morogoro, na anatarajia kukiongoza kikosi chake cha Hard Rock kwenye mshike mshike wa ligi ya Zanzibar ambao umepangwa kuanza Oktoba Mosi.

Video: Saida Karoli awaweka katika 'Kichaka' Belle 9 na G Nako
Mahujjaji 35 waaga dunia wakifanya ibada Makkah