Aliyewahi kuwa kocha wa Simba, Tanzania Prisons na klabu kadhaa nchini, ambapo sasa ni bosi wa Njombe Mji ya Ligi Daraja la Kwanza, David Mwamwaja, amefanyiwa upasuaji usiku wa kuamkia jana na hali yake inatia matumaini kidogo.

Hatua hiyo imekuja baada ya kocha huyo kuanguka na kujigonga kichwani ambapo alipata hitilafu, ambapo alipata matibabu ya awali kwenye Zahanati kabla ya kuhamishiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Mke wa kocha huyo, Maria Mwamwaja, amesema mumewe amefanyiwa oparesheni lakini tatizo litakuwa la kudumu japokuwa ameanza kutambua watu tofauti na awali ambapo hakuwa na uwezo huo.

“Naomba Watanzania wamsaidie kwa sababu kuna baadhi ya fedha tunadaiwa hapa hospitalini na bado anahitaji matibabu zaidi na uangalizi, amelazwa wodi ya Sewahaji chumba namba 18,” alisema mama huyo.

Watanzania watakaoguswa kumsaidia na kumchangia kocha huyo watume michango yao kupitia namba ya mkewe, Maria Benjamin Mwamwaja 0714621554.

Chanzo: salehjembe

Mchezaji Wa Chelsea Asakwa Na Polisi
Lembeli Aeleza Hatma Yake Baada Ya Kushindwa, Ajibu Tetesi Juu Yake