Kocha Mkuu wa Timu ya taifa ya Tanzania Taifa stars, Emmanuel Amunike amewaondoa kikosini wachezaji wa Simba SC kwa kosa la kutoripoti kambini isipokuwa Golikipa Aishi Manula ambaye amesharipoti.

Akizungumza na waandishi wa habari Katiba Mkuu, Wilfred Kidao amesema kuwa uamuzi huo umetolewa baada ya raisi wa TFF Walice Karia kuridhia maamuzi hayo yaliyofanywa na  Kocha Amunike.

‘’Aliniomba kwenye kikao cha dharula tukawa tumekwenda kule kwaajili ya kusikiliza maamuzi yake, baada ya kujadiliana na mwalimu alitoa mapendekezo yake, kwa hiyo tuliwasiliana na raisi kuhusu msimamo wa mwalimu na raisi wa TFF ameahidi kumsapoti Mwalimu kwa asilimia mia kwa kile anachoona kinafaa’’ amesema Kidau.

Wachezaji hao walitakiwa kuripoti kambini siku ya jumatatu ya wiki hii baada ya mchezo wa Simba dhidi ya Mbeya City lakini hawakufanya hivyo.

Aidha, Wachezaji hao ni pamoja na nahodha wa klabu hiyo John Bocco, Jonas Mkude, Erasto Nyoni, Shiza Kichuya, Jonas Mkude, Shomali Kapombe na Hassan Dilunga.

Wakati huo huo, Kocha huyo amewawaita wachezaji wengine kuchukua nafasi za wachezaji hao wa Simba, wachezaji walioitwa  ni pamoja na Paul Ngalema, Salumu Kimenya, David Mwantika, Salumu Kihimbwa, Ali Abdulkadir, Kevin Sabato na Frank Damayo.

Hata hivyo, kwa upande wa viongozi wa klabu ya Simba Meneja, Richard Robart pamoja na kaimu katibu mkuu Hamis Kisiwa wamepelekwa kwenye kamati ya maadili ya shirikisho la Soka (TFF) kwa kushindwa kutimiza wajibu wao.

Yaya Toure afanya vipimo London, kusajiliwa kimya kimya
Ndalichako: Hatutoi mabilioni ya fedha watoto wakapoteze maisha shuleni