Lazima ujue Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van Der Pluijm si mtu wa mzaha.

Jana alichukua uamuzi wa kumshusha kiungo wake kinda Geofrey Mwashiuya katika kikosi B.

Halafu wakati wengine wakishangaa, akampandisha James Msuva Yanga A.

Pluijm ambaye ni kipa wa zamani wa timu ya taifa ya Uholanzi, ameonyesha si mtu wa mchezo wala mzaha.

Kocha huyo amesisitiza kwamba anataka watu wanaojitambua ndani ya kikosi chake. Yanga imekuwa ikiendelea na mazoezi kwenye Uwanja wa Boko Veterani jijini Dar es Salaam.

Huenda hilo likawa mfano kwa makocha wengine.

Ripoti: Mawaziri wa JK watajwa kuhusika Ufisadi wa Mabilioni
Kinda La Kiafrika Lawanyima Usingizi FC Barcelona