Meneja wa Majogoo wa Jiji ‘Liverpool’ Klopp Jurgen amesema bado kikosi chake kinacheza soka lenye ubora na ndio maana walifanikiwa kuibanjua Leeds United 6-1 mwanzoni mwa juma hili.

Liverpool ilipata ushindi katika mchezo wa huo Ligi Kuu ya England (EPL), uliochezwa katika Uwanja wa Elland Road nchini humo.

Katika mchezo huo, Mo Salah na Diogo Jota kila mmoja alifunga mabao mawili wakati mengine yakifungwa na Coady Gakpo na Darwin Nunez huku bao la Leeds likifungwa na Luis Sinistera.

Klopp amesema kikosi chake kilipambana kiume na kufanikiwa kupata matokeo makubwa, huku kikionesha kiwango bora zaidi katika mchezo huo kuliko michezo mingine iliyotangulia msimu huu 2022/23.

“Nina furaha sana kuhusu huu mchezo. Nafikiri ni mchezo bora zaidi tuliocheza msimu huu, katika maeneo tofauti,” amesema Klopp.

Pamoja na ushindi huo, Klabu ya Liverpool inashika nafasi ya nane katika msimamo wa Ligi Kuu ya England kwa kuwa na alama 47, baada ya kucheza michezo 30 hadi sasa, huku Leeds United ikishika nafasi ya 16 ikiwa na alama 29 baada ya kushuka dimbani mara 31.

Katika Ligi Kuu ya msimu huu Liverpool imebakisha michezo minane ambayo ni dhidi ya Nottingham Forest, West Ham United, Tottenham Hotspur, Fulham, Brentford, Leicester, Aston Villa na Southampton.

Leeds imebakisha michezo dhidi ya Fulham, Leicester City, AFC Bournemouth, Manchester City, Newcastle United, West Ham United na Tottenham Hotspur.

PICHA: JK akutana na wanariadha Gabriel Geay na Wence Tarimo mjini Boston, MarekaniPICHA:
Mkutano wa Azimio la Umoja waahirishwa