Meneja wa FC Barcelona Ronald Koeman amekiri kuona mabadiliko makubwa kwenye kikosi chake, tofauti na ilivyokua msimu uliopita ambapo Barca hawakufanya vizuri kwenye michuano ya ndani na nje ya Hispania (La Liga).

Koeman ametoa kauli hiyo kufautia kikosi chake kuwa na muendelezo mzuri kwenye michuano ya ndani (La Liga) na nje ya Hispania (Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya).

Kocha huyo kutoka  kutoka nchini Uholanzi amesema: “Hivi karibuni, tuna ufanisi zaidi, katika safu ya ulinzi bado tunaweza kuboresha, lakini tuko kwenye njia sahihi na tunatumahi tunaweza kuendelea kama hivi.”

“Tofauti ni kwamba timu imekuwa na ufanisi katika michezo. Ni mabadiliko makubwa ikilinganishwa na mwanzo wa msimu. Njaa ambayo tunayo, lazima ukubali.

“Jambo muhimu zaidi ni kufika hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa, lakini ikiwa utashinda sita kati ya sita itakuwa hatua ya kihistoria.”

FC Barcelona imefanikiwa kushinda michezo mitano ya kundi G kwenye michuano ya Ligi ya mabingwa barani Ulaya, huku wakishinda mabao matatu kwa sifuri dhidi ya Ferencvaros.

Endapo FC Barcelona watapata nafasi ya kushinda michezo sita katika michezo ya makundi kwa mara ya kwanza tangu msimu wa 2002-03 watakapowavaa na mabingwa wa Italia Juventus FC, kwenye dimba la Camp Nou, juma lijalo.

Kwa upande wa Ligi ya Hispania (La Liga), FC Barcelona kinapambana vilivyo, lakini wapo nyuma kwa alama 10 dhidi ya Real Sociedad, wanaoongoza msimamo wa ligi hiyo kwa sasa.

FC Barcelona inashika nafasi ya 12 kwa kufikisha alama 14, lakini ina michezo miwili mkononi  baada ya kupoteza mara tatu na sare mbili kati ya tisa ya ufunguzi.

Sherehe za Uhuru zaahirishwa
Jengo la mama na mtoto Mwananyamala kuanza kazi