Mwanamuziki nguli wa dansi Afrika, Antoine Agbepa Mumba maarufu kama Koffi Olomide amehukumiwa kutumikia kifungo cha nje kwa muda wa miaka miwili baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka mmoja wa wanenguaji wake akiwa mwenye umri wa miaka 15.

Olomide ametakiwa kumlipa msichana huyo shilingi Milioni 13 pesa ya kitanzania kama fidia ya kutenda kosa hilo.

Mbali na hilo mwanamuziki huyo ametakiwa kulipa faini ya shilingi milioni 13 pesa ya kitanzania kwa kosa la kuingiza wasichana watatu nchini Ufaransa kinyume na sheria.

Wanenguaji wake wanne wametoa ushaidi mahakamani wakidai kuwa bosi wao amekuwa akiwasumbua na kuwanyanyasa kingono mara nyingi kati ya mwaka 2002 na 2006 , wamesema matukio hayo ya unyanyasaji yamekuwa yakifanyika wakiwa nchini Congo na Ufaransa.

Aidha msanii huyo maarufu wa muziki wa rumba barani Afrika amekuwani mtu wa matukio na skendo mbalimbali kama ambavyo rekodi zake zinasoma hapa chini;

Mnamo mwaka 2018, huko Zambia, Olomide alitiwa mbaroni baada ya kuwaletea fujo wapiga picha nchini humo.

Mwaka 2016, alitiwa mbaroni baada ya kumletea fujo na kutaka kumpiga mmoja ya wanenguaji wake akiwa nchini Kenya.

2012 huko Kaunti ya Congo alimfanyia fujo mtayarishaji wa muziki wake hali iliyopelekea atiwe ndani kwa muda wa miezi mitatu.

Na 2008 alishutumiwa kwa kumpiga mtu wa camera kutoka televisheni ya RTGA na kuvunja kamera yake wakiwa kwenye tamasha.

 

 

 

Zitto afunguka Maalim Seif kutimba ACT-Wazalendo, ''Asante viongozi wa Chadema''
Video: Maalim Seif rasmi ACT, Mbuge mwingine upinzani matatani