Mataifa ya Hispania na Ureno yameingia mkataba maalumu wa kuunda muungano wa kujipigia chapuo kuandaa Fainali za Kombe la Dunia (FIFA WORLD CUP) mwaka 2030.
Awali katika muungano huo pia walikuwepo Morocco kutoka Afrika lakini Raisi wa Shirikisho la soka Barani Ulaya UEFA, Aleksander Ceferin alipinga uwepo wa Morocco kwa kuwa nchi hiyo ipo bara tofauti na Ulaya.
“Siafiki kombe la Dunia kufanyika katika mabara mawili tofauti. Tuingie katika kampeni hizi kama Ulaya na Afrika nao wataingia kama wao ili kuweka rekodi sahihi za mabara yetu kuandaa michuano hii adhimu duniani”
Serikali ya Morocco imesema hilo haliwakatishi tamaa kuitafuta nafasi hiyo ya kuandaa michuano hiyo wao kama wao.
Kumbe Ntibazonkiza, amecheza Ulaya!
“Wenzetu Afrika kusini waliweza mwaka 2010 pia nasi tunaweza kuirudisha michuano hiyo Afrika endapo tutapata fursa hiyo” – Alisema waziri mkuu wa nchi hiyo
Ukiwaondoa Morocco na umoja wa Uhispania na Ureno katika kampeni hizo, pia taifa la Uingereza lipo katika kinyang’anyiro hicho cha kuandaa michuano ya Kombe la Dunia 2030. Wagombea wengine ni kutoka Amerika ya kusini mataifa ya Argentina, Paraguay, Uruguay na Chile ambao pia wanataka kuandaa michuano hiyo kwa pamoja.