Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans wamepangwa kucheza na klabu ya Club Africain ya Tunisia katika mchezo wa Hatua ya Matoano Kombe la Shirikisho Barani Afrika kupitia Droo iliyopangwa leo Jumanne (Oktoba 18) Mchana.
Young Africans iliangukia Kombe la Shirikisho Barani Afrika, baada ya kutolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Barani Afrika na Mabingwa wa Soka nchini Sudan Al Hilal, iliyoibuka na ushindi wa jumla wa 2-1.
Mchezo wa Mkondo wa Kwanza utashuhudia Young Africans ikicheza nyumbani Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es salaam, Jumatano (Novemba 02), kabla ya Mchezo wa Mkondo wa pili ambao utapigwa Uwanja wa Olympique de Radès uliopo mjini Tunis, Jumatano (Novemba 09).
Hii itakua mara ya pili msimu huu kwa Club Africain ya Tunisia kuja Tanzania, baada ya kucheza na Kipanga FC ya visiwani Zanzibar katika mchezo wa Hatua ya kwanza ya Kombe la Shirikisho.
Mchezo wa Mkondo wa Kwanza ikicheza dhidi ya Kipanga FC kwenye Uwanja wa Amaan Unguja, Club Africain iliambulia sare ya bila kufungana, na iliporejea nyumbani kwao Tunisia kwa ajili ya Mkondo wa Pili, ilipata ushindi mnono wa 7-0.
Michezo Mingine ya Hatua ya Mtoano Kombe la Shirikisho Barani Afrika iliyopangwa leo Jumanne (Oktoba 18).
Washindi wa Michezo ya Mtoano watatinga Hatua ya Makundi Kombe la Shirikisho Barani Afrika msimu huu 2022/23.