Nahodha na beki wa klabu ya Man City, Vincent Jean Mpoy Kompany, amesema kikosi chao kina njaa ya kusaka mafanikio kwa msimu huu, baada ya kuonyesha hali ya kusuasua msimu uliopita na kujikuta wakimaliza bila kutwaa taji lolote.

Kompany, ametangaza njaa ya kikosi cha Man City, alipokua kwenye mkutano na waandishi wa habari uliokua unazungumzia mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya ambao utashuhudi, mabingwa wa soka nchini Italia Juventus wakifunga safari kuelekea Etihad Stadium.

Beki huyo mwenye asili ya jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, amesema tayari wameshaonyesha ni vipi walivyo na njaa ya mafanikio kwa msimu huu kupitia michezio ya ligi kuu ya soka nchini England, ambapo mpaka sasa wameshacheza michezo minne na kufanikiwa kushinda yote.

Amesema hali hiyo inatoa nafasi kwa kila mmoja wao kikosini kuamini hakuna litakalowashinda kwa msimu huu, ambao unatazamwa kama kipimo kwa klabu kadhaa za nchini England pamoja na barani Ulaya kwa ujumla.

Akiwazungumzia wapimnzani wao, Kompany amesema Juventus ni klabu yenya mafanikio na inajua nini maana ya kupambana, hivyo kiu yao ya mafanikio haiwapi fursa ya kuwadharau zaidi ya kuamini wana uwezo wa kutumia mbinu mbalimbali za kuwashinda.

Amesema kitendo cha kufika katika hatua ya fainali msimu uliopita kabla ya kufungwa na FC Barcelona kilichoonyeshwa na Juventus ni kigezo tosha cha kuwapa heshima, japo anaamini kikosi cha Man City hakina shaka na mpambano wa hii leo.

Katika mchezo huo Man City watamkosa mshambuliaji wao kutoka nchini Argentina Sergio Leonel Agüero Del Castillo, kutokana na majeraha aliyoyapata mwishoni mwa juma lililopita wakati wa mchezo wa ligi ya nchini England dhidi ya Crystal Palace.

Siri nyingine 5 Kubwa Za Mafanikio bila Utegemezi hizi hapa
Picha Ya Lowassa Yasababisha Kifo