Wachezaji wa zamani wa wababe wa sasa wa EPL Manchester city Muhispania David Silva na kitasa cha zamani cha Kibelgiji Vicent Kompany wamejengewa sanamu na timu hiyo yenye maskani yake katika jiji la Manchester

Ubunifu wa sanamu hizo zenye nakshi mbalimbali zimebuniwa na mshindi wa tuzo za uchangaji sanamu duniani bwana Andy Scott ,ambapo sanamu hizo zitawekwa upande wa Mashariki mwa uwanja wa Etihad

Silva ambaye amecheza zaidi ya michezo 400 akiwa City kwenye EPL akidumu kwa misimu 10 tangu asajiliwe kutoka Valencia mwaka 2010 amesema kuwa anajihisi mwenye furaha baada ya kujengewa sanamu na wakali hao walio chini ya Pep kwa sasa

Huku mkongwe mzee wa hizi kazi Vincent Kompany ameweka wazi furaha yake kuwa ushabiki wake na kazi aliyoifanya itaonekana kwa urahisi na familia kwa kuwa watoto wake ni wakazi na mashabiki wa Manchester city

Young Africans yawachomoa wachezaji kambini Stars
Tuisila Kisinda atambulishwa rasmi RS Berkane