Jumuiya ya maridhiano Tanzania inatarajia kufanya kongamano la maombi Jijini Dodoma litakalo wakutanisha viongozi mbalimbali wa kitaifa kwaajili ya kuombea uchaguzi mkuu litafanyika agosti 24,2020

Mwenyekiti wa jumuiya ya maridhiano Sheikh Alhad Mussa Salum amesema lengo la kongamano hilo ni kuombea uchaguzi pamoja na kuwaweka pamoja viongozi wa kisiasa na kulinda amani ya nchi kwa ujumla.

Yapo maisha baada ya uchaguzi kwa maana hiyo jumuiya ya maridhiano kwa kufanya kwake kazi kuwaunganisha viongozi wa dini pamoja na serikali ni lazima tuhakikishe tunasimamia misingi ya haki, upendo, mshikamono na amani katika nchi yetu”amesema Shekh Salum

Kwa upande wake mwenyekiti wa maridhiano mkoa wa Dodoma Mchungaji Evanc e Lucas Chande wa kanisa la EAGT Nazael Ipagala amesema kuwa kongamano hilo linalenga kwajenga watanzania wote kuendelea kuwa wamoja.

Kadharika mwenyekiti wa maridhiano kwa upande wa kina mama Pili Yomba amewasisistiza wakina mama kujitokeza kwa wingi kuhudhuria katika kongamano hilo kwa lengo la kujifunza mambo mengi na ya muhimu.

Viongozi wa dini muwakemee wanasiasa kwa hili- IGP Sirro
Madaktari waliokwama Cuba kurejea