Korea Kusini imesema kuwa kuna uwezekano wa Korea Kaskazini kuwa katika mipango ya kufanya majaribio zaidi ya makombora ya masafa marefu.
Baada ya Korea Kaskazini kufanya jaribio la bomu la nyuklia mwishoni mwa wiki Korea Kusini imejibu kwa kufanya majaribio ya kurusha makombora kwa kutumia ndege na makombora ya kutoka ardhini.
Korea Kusini imesema kuwa imefanya majaribio matano kama majibu ya jaribio la nyuklia la Korea Kaskazini ambayo imekuwa ikifanya majaribio hayo mara kwa mara.
Korea Kaskazini najiandaa kufanya majaribio zaidi ya kurusha makombora huku Marekani ikiwa imetoa onyo kuwa tishio lolote kwake na kwa washirika wake litakalofanywa na Korea Kaskazini litajibiwa vikali kijeshi.
-
Marekani yatishia kuitwanga Korea Kaskazini
-
Trump apanga kuwaelewesha Korea Kaskazini kwa kitu kimoja tu
-
Kenyatta: Sikubaliani na uamuzi wa Mahakama lakini…
Kutokana na taarifa hizo baraza la ulinzi la umoja wa mataifa linatarajiwa kufanya kikao cha dharura leo kujadili hatua za kuchukua dhidi ya Korea Kaskazini.
“Tunaendelea kuona dalili za uwezekano wa makombora zaidi, Korea Kaskazini itarusha kombora la masafa marefu” alisema Chang Kyung-soo ambaye ni afisa kutoka wizara ya ulinzi ya Korea kusini.
Wizara ya ulinzi ya Korea kusini pia ililiambia bunge la nchi hiyo kuwa huenda Marekani ikapeleka manowari wa nyuklia ya kubeba ndege katika rasi ya Korea.